Lava lava – Utatulia lyrics

1337 Views
Loading...

Stanza 1

Kiangazi masika ukichanganya

Vyote vikashuka kwangu vitanielemea

Nitakosa pa kushika nitavavanya

Wewe ndo mwandani wangu nilokuzoea

Mtunza vyangu visiri, mwenye kunisitiri, fundi mitambo

Kinga yangu ya mwili, usiyelipa bili, kuchoma chango

Simtaki kafiri,  jangili,  mwingi wa mambo

Moyo akaukatilli, nikondeshe mwili, ajifanye rambo

Bridge

Si unajua, dalili ya mvua mawingu

Ikitaka kunyesha, huwa yanatanda

Nami si unajua, nimeumbwa na wivu

Kidogo tu presha, yanishuka yapanda

Niahidi kama

Chorus

(Utatuliaaaa)

Baby niahidi kama

(Utatuliaaaa)

Mmmh  nisibaki nikashika tama

(Utatuliaaaa)

Baby niahidi kama

(Utatuliaaaa)

Mmmh wasiniibie changama

Stanza 2

Maneno yangu si biblia, wala masaafu, tuseme usibadili

Jichunge kipenzi changu, Unanisikia usicheze rafu, yatimie waliotabiri

Iyeeeeeh yeye yeeeee

Usijifanye Ronaldinho, penzi utie mbwembwe, utahaaribu

Visokolokwinyo, wakupitie denge, kukujaribu

Kina Kapachino wakakutia wenge, kwa vizabibu

Wakugongeshe mvinyo, ukaota mapembe, iwe aibu

Bridge

Si unajua, dalili ya mvua mawingu

Ikitaka kunyesha, huwa yanatanda

Nami si unajua, nimeumbwa na wivu

Kidogo tu presha, yanishuka yapanda

Niahidi kama

Chorus

(Utatuliaaaa)

Baby niahidi kama

(Utatuliaaaa)

Mmmh  nisibaki nikashika tama

(Utatuliaaaa)

Baby niahidi kama

(Utatuliaaaa)

Mmmh wasiniibie changama

Outro

Yaani kama

(Ukitulia tulia)

Sitathubutu macho kupepesa

(Ukitulia tulia)

Ukinipa kiduchu nitatosheka

(Kama ukitulia tulia)

Sitofuata nguruchu niende teseka

(Ukitulia tulia)

Eeeh nami nitatulia

 

Watch the Official Lava lava – Utatulia video here:

https://www.youtube.com/watch?v=gD0ZjiHSCOw

Find also Lava lava – Gundu lyrics here:

https://mutaha.com/entertainment/lava-lava-gundu-lyrics/

Loading...

Leave a Reply

%d bloggers like this: