Lava lava – Tuachane lyrics

1380 Views
Loading...

Intro

Aaaaaahh aaaahh aahh

Aaaaaahh aaaahh aahh

Stanza  1

Kama imeshindikana kunirudia isiwe taabu

Usiuforce moyo kupenda usipostahili

Ya nini kung’ang’ania nishachoka kuwekwa sub

Siwezi ooh na mapenzi nishaghaili

Tena niko tayari vipigwe vinumbi kengere kwa sherehe

 Kinaghaubagha mbele ya umati tuachane

Na kama hautojali tuite waumini mapadri na masheikh

Yaishe labda sa kwa nini tutesane

Kweli we ndo nikupendae ila unanipa ghadabu Jina

Tusitoane nyongo

Na kama umenichoka niache kistarabu Jina

Usinipe chongo mieehh

Bridge

Mwili umebaki kongoro nyama sina ni mifupa

Naiona ndomboro kabisa siwezi furukuta

Penzi kiporo limeshachina linanuka

Huishi kokoro purukushani kutwa kucha iyeee

Chorus

(Bora tuachane)

Bora tuachane siwezi

(Bora tuachane)

Yamenishinda mapenzi

(Mi naona bora tuachane)

 Eeh tuachane siwezi

(Bora tuachane)

Yamenishinda mapenzi

Stanza  2

Ni dhahiri kisima kimekauka maji

Ndo maana naona kata sina maana tena

Nilifikiri mi gonjwa langu limepata mponyaji

Umeniongezea homa mwili wote wantetema

Mi naona basi labda si riziki yangu

Kama hunitaki acha tu niende zangu

Ya nini mishikaki ntatafuta boda yangu

Nijinafasi niipande peke yangu

Bridge

Mwili umebaki kongoro nyama sina ni mifupa

Naiona ndomboro kabisa siwezi furukuta

Penzi kiporo limeshachina linanuka

Kuishi kokoro purukushani kutwa kucha iyeee

Chorus

(Bora tuachane)

Bora tuachane siwezi

(Bora tuachane)

Yamenishinda mapenzi

(Mi naona bora tuachane)

 Eeh tuachane siwezi

(Bora tuachane)

Yamenishinda mapenzi

Watch the Official Lava lava – Tuachane video here:

https://www.youtube.com/watch?v=BJ9FLAnEUg4

Find Lava lava biography, age, relationships and songs here:

https://mutaha.com/entertainment/lava-lava-biography-age-relationships-and-songs/

Loading...

Leave a Reply

%d bloggers like this: