Lava lava – Kilio lyrics

1018 Views
Loading...

Stanza  1

Mmmh  mmh

Hali yangu mbaya, anifikiria akipata muda (akipata muda)

Moyo ameshaugawa, pakacha penzi linavuja (limeshavuja)

Mwenzie ninapagawa nahisi uchizi, na network haisomi

Mmmh

Anayofanya si sawa nakosa usingizi, mwilini miwasho na vichomi

Eeee iiiii

Bridge

Mwambie, kuachwa mateso nasulubiwa

Mwenzie, yatima wa penzi mwana mkiwa

Ooh mie, mapenzi ugonjwa nimezidiwa

Ni yeye, mwengine sioni kunitibia

Chorus

(Kilio oo kilio oo)

Kilio na penzi langu

(Kilio oo kilio oo)

Huruma hana

(Kilio oo kilio oo)

Yarabi Mola wangu

(Kilio oo kilio oo)

Japo simama

Stanza  2

Ye ndio barafu, niliemlia yamini

Pemba karafu, marashi yangu mwilini

Utamu wa dafu, mbona ameuitia kwinini

Amenichezea rafu, penzi amelikafini

Eeeeh

Ye anajivinjali mwenzake nadoda

Napata tu habari anagawa uroda

Tetemeko moyo kupenda uoga

Najiepusha mbali kukwepa vihoja

Bridge

Mwambie, kuachwa mateso nasulubiwa

Mwenzie, yatima wa penzi mwana mkiwa

Ooh mie, mapenzi ugonjwa nimezidiwa

Ni yeye, mwengine sioni kunitibia

Chorus

(Kilio oo kilio oo)

Kilio na penzi langu

(Kilio oo kilio oo)

Huruma hana

(Kilio oo kilio oo)

Yarabi Mola wangu

(Kilio oo kilio oo)

Japo simama

Outro

Moyo wangu bado

(Mteke mteke)

Asinikondeshe mwenzake bado

(Mteke mteke)

Asinizeeshe mi mdogo bado

(Mteke mteke)

Asinokomaze roho moyo bado

(Mteke mteke)

 

Watch the Official Lava lava – Kilio video here:

https://www.youtube.com/watch?v=e-2J0EZ_7ss

Find also Lava lava – Teja lyrics here:

https://mutaha.com/entertainment/lava-lava-teja-lyrics/

Loading...

Leave a Reply

%d bloggers like this: