Lava lava – Gundu lyrics

1260 Views
Loading...

Stanza 1

Mmmmmh   eeeh

Naona maajabu, kinanizonga kizaazaa

Kila mahesabu, ninayopiga yanakataa

Nahisi mababu, mizimu yao imechachamaa

Au sina thawabu, Mola nionyeshe nyota ya jaa

Eeeeeh

Kulia nimelia, nikamaliza leso, nimekosa kipenda roho

Mi nikasubiria, huwenda akaja kesho, nilipodososa kote ngoma droo

Chorus

Mwenye mapenzi atokee

(Anitetee)

Joto pepee

(Anipepee)

Niwe mtoto tetee

(Ooh tetee)

Anidekee

(Dekee dekee)

Eeeeh mi niepuke gundu

(Oooh gundu)

Penzi linanichachia gundu

(Oooh gundu)

Nuksi imenishukia gundu

(Oooh gundu)

Penzi chachia gundu

(Oooh gundu)

Nuksi imenishukia gundu

 Stanza 2

Ama sina bahati, jini gani kanivaa, asio na jema kwangu

Ninaemtaka simpati, vioja tu na karaha, yani vanguvangu

Mieee iyeeeh

Nahisi nalala na bundi, najisonyasonya

Penzi sasa bila hudi, ni maronyaronya

Nishapangwa kwa makundi, nikabonywabonywa

Licha ya wangu ufundi, nikapokonywa

Mi nina taabu

Chorus

Mwenye mapenzi atokee

(Anitetee)

Joto pepee

(Anipepee)

Niwe mtoto tetee

(Ooh tetee)

Anidekee

(Dekee dekee)

Eeeeh mi niepuke gundu

(Oooh gundu)

Penzi linanichachia gundu

(Oooh gundu)

Nuksi imenishukia gundu

(Oooh gundu)

Penzi chachia gundu

(Oooh gundu)

Nuksi imenishukia gundu

 

Watch the Official Lava lava – Gundu video here:

https://www.youtube.com/watch?v=bmVXA2CXitI

Find also Lava lava – Nitake Nini lyrics here:

https://mutaha.com/entertainment/lava-lava-nitake-nini-lyrics/

Loading...

Leave a Reply

%d bloggers like this: