Harmonize – Matatizo lyrics

1223 Views
Loading...

Stanza 1

Alfajiri imefika, anga inang’aa

Mvua inaanza katika,  ghafla tumbo la njaa

Naweka sauti kwa spika, nipate umbea wa Dar

Mara simu inaita, jina la Uncle Twaha

Akisema, mama yu hoi kitandani, kama si wa leo wa kesho

Na kupona sidhani, upate japo neno la mwisho

Pre-chorus

Mi ndo mtoto wa pekee, nyumbani wananitegemea

Mdogo wangu wa kike, hali duni alishaga olewa

Tizama jasho langu la mnyonge, kipato hakikidhi mahitaji

Napiga moyo konde, Yarabi Mola ndo mpaji

Chorus

Matatizo

(Matatizo yatakwisha lini, matatizo kila siku mimi)

Ewe Mola

(Matatizo yatakwisha lini, japo likizo nifurahi na mimi)

Stanza 2

Mola aliniumba na subira, imani pekee ngao yangu

Mbona nishasali sana, ila mambo bado tafalani

Mama kanifunza kikabila, nikonde sana haini yangu

Tena nijitume sana, na vya watu nisivitamani

Hata mpenzi nilo nae, najua siku atanikimbia

Itanitesa ye ndo nguzo

Zile ngoja kesho badae, atazichoka kuzivumilia

Anakosa hata matuzo

Bridge

Ona, nadaiwa kodi nilipopanga, nashinda rodi nikihanda

Nishapiga hodi kwa waganga (kwa kuhisi narogwa)

Nikauza maji na karanga, nikawa dobi kwa viwanda

Ila kote ziro ni majanga (mtindo mmoja)

Pre-chorus

Mi ndo mtoto wa pekee, nyumbani wananitegemea

Mdogo wangu wa kike, hali duni alishaga olewa

Tizama jasho langu la mnyonge, kipato hakikidhi mahitaji

Napiga moyo konde, Yarabi Mola ndo mpaji

Chorus

Matatizo

(Matatizo yatakwisha lini)

Ewe Mola

(Matatizo kila siku mimi)

Jamani matatizo

(Matatizo yatakwisha lini, japo likizo nifurahi na mimi)

Matatiiiiiizo

(Matatizo yatakwisha lini, matatizo kila siku mimi)

Jama matatizo

(Matatizo yatakwisha lini, japo likizo nifurahi na mimi)

Watch the Official Harmonize – Matatizo video here:

https://www.youtube.com/watch?v=VMyRIff0OJg

Find Harmonize feat Sarkodie – DM Chick lyrics here:

https://mutaha.com/entertainment/harmonize-feat-sarkodie-dm-chick-lyrics/

Loading...

Leave a Reply

%d bloggers like this: