Stanza 1: Harmonize
Kutwa kidomo wazi, nikifuta na machozi
Huku namuomba Mola unitoke moyoni
Ila ndo siwezi, nakesha ka mlinzi
Maana hata nkilala unaniijia ndotoni (Lato)
Asante kwa kuniumiza
Nimejifunza mengi, mwanzo sikuyajua (Katu)
Naapa kutolipiza
Ila mwambie mapenzi abaki kuyasikia
Nakumbuka maneno yako
Hutonikimbia utabaki nami
Tena ukala na viapo Taurat Biblia, leo sikuoni
Chorus: Harmonize
Ila mwenzako bado
(Bado bado, bado bado)
Mwambie bado
(Bado bado, sijapona)
Ila mwenzako bado
(Bado bado, bado bado)
Mmmh bado
(Bado bado, sijapona)
Mi sijapona roho
Stanza 2 : Diamond Platnumz
Mola nishike mkono Baba Muumba
Haya ninayoyaona, simanzi
Yaani bora jicho mchanga ningefumba
Huenda ningeshapona, maradhi
Maumivu yangu, hayawezi kupona kwa vidonge
Sababu panaponichoma, nikipapasa sipaoni
Kweli peke yangu, umeniacha na unyonge
Kabisa wakanipokonya tonge langu mdomoni
Pre Chorus: Diamond Platnumz
Ooh nana nakumbuka maneno yako
Hutonikimbia, utabaki nami
Ooh mi ndo mwili, mi roho yako
Yaani umetimia, mbona sikuoni
Chorus: Harmonize
Ila mwenzako mimi
(Bado bado) Mmmh (bado bado)
Mwambie bado
(Bado bado, sijapona)
Ila mwenzako bado
(Bado bado bado bado)
Mmmh bado
(Bado bado, sijapona)
Bridge : Diamond Platnumz
Ile roho yangu mama (Ibebe)
Inanidondoka (Ibebe)
Iokote mama (Ibebe, Chaukucha nsije zima)
Oooh roho yangu (Ibebe)
Inanidondoka (Ibebe)
Njoo unishike mama (Ibebe, Chaukucha nsije zima)
Aaai wewe (Ibebe)
Watanizika mama (Ibebe)
Mwenzio taabani (Ibebe, Chaukucha nsije zima)
Bridge : Harmonize
Mmh masikini pendo langu (Ibebe)
Linanidondoka (Ibebe)
Niokote mama (Ibebe, Chaukucha nsije zima)
Outro
Ibebe, ibebe
Ibebe, Chaukucha nsije zima
Ibebe, ibebe
Ibebe, Chaukucha nsije zima
Watch the Official Harmonize ft. Diamond Platnumz – Bado video here:
https://www.youtube.com/watch?v=M6PJp1p6BLg
Find Harmonize ft. Koredo Bello – Shulala lyrics here:
https://mutaha.com/entertainment/harmonize-ft-koredo-bello-shulala-lyrics/
No Responses