Diamond Platnumz – Sikomi lyrics

313 Views
Loading...

These are the lyrics to the bongo flava song Sikomi by Diamond Platnumz

Stanza 1

Wanasemaga mapenzi safari, unavyopita ndo jinsi unajongea

Ila niendako ni mbali, sijui ka ntafika sababu natembea

Niliposikiaga Habari, yakisifika nikakesha nangojea

Akabariki Jalali, na nikawika muziki nikauotea

Ile pruu mpaka Macca, nikadandiaga Bongo movi

Kumbe mapenzi hayataki haraka, ni kama tango natia tu chumvi

Mwenzenu nikaoza haswa, na kujitia kitandani mjuzi

Eti nataka fukuza paka, badala ya mbwa nikafuga mbuzi

Wivu ukanifanya,  nikagombana na marafiki

Ugomvi na mamangu akiniambia siambiliki

Bridge

Moyo ukanambia Nasibu sasa mapenzi basi

Ila nang’ang’ania najaribu kuipinga nafsi

Esma ananiambia mdogo wangu mapenzi basi

Ila nang’ang’ania, nikiumizwa na huyu kesho nina mwingine


Chorus

Ooh mbona sikomi, sikomi, sikomi

Licha ya mateso haya

Najiuliza

Ooh Sikomi, sikomi, sikomi

Licha ya mateso haya

Stanza 2

Aliyonifanyia wa centro, haki ya Mungu siyawezi sema

Ila nimejifunza kesho,  nisiwaamini wacheza cinema

Moyo walinipatia mateso, siwezi kumeza siwezi tema

Ndio maana sikushanga ile ghafla, toka CCM kwenda CHADEMA

 

Wanasema kitanda ukitandika sharti ukilalie

nikajitia ukamanda yatakwisha,  acha nivumilie,

kila kiza kikitanda, ndo visa machozi me nilie,

penzi yakatia parapanda, kuwaita waje washambulie,

acha na penny we dari, nilio muhongaga gari

aliponambia ana mimba, mwisho wa siku akaichomoa chali

Mola akanitunuku Zari, akanizalia dume na mwali

Niliyvo mjinga nikacheat aibu mpaka, kwa vyombo vya habari

Bridge

Moyo unanambia, Nasibu sasa mapenzi basi

Ila nang’ang’ania, najaribu kuipinga nafsi

Lizer ananiambia, simba mapenzi basi

Ila nang’ang’ania, nikiumizwa na huyu kesho nna mwingine

Chorus

Ooh mbona sikomi, sikomi, sikomi

Licha ya mateso haya

Eh Nishafumania

oh sikomiii

Nikafumaniwa mimi

Sikomi

Nishagombana na watu

Sikomi

Licha ya mateso haya

Mateso haya


Loading...

Leave a Reply

%d bloggers like this: